Wizara ya ardhi, maji, nishati na mazingira imeanza taratibu za kupeleka huduma za umeme katika kisiwa cha Fundo kisiwani Pemba.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi waziri wa wizara hiyo Salama Abodu  amesema upelekaji wa umeme katika kisiwa hicho utaanza mwezi ujao kwa kuweka nguzo.

Amewataka wananchi kutokuwa na wasiwasi juu ya utekelezaji wa ahadi ya serikali ya kupeleka umeme katika kisiwa cha Fundo

Miundo mbinu ya huduma za umeme katika kisiwa cha Fundo unatarajiwa kupita chini ya bahari na utagharimu mamilioni ya fedha.