Serikali yajadili ukarabati wa kituo cha afya Kitogani Kusini Unguja

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  kupitia Wizara ya afya  imeombwa kuchua hatua za haraka kukifanyia matengenezo kituo cha afya cha Kitogani ili kuwarahisishia wananchi upatikanaji wa huduma za matibabu kwa  urahisi.

Akiuliza swali katika kikao cha baraza la wawakilishi, Mwakilishi wa jimbo la Paje Jaku Hashim Ayoub  amesema ni muda mrefu  serikali imetoa ahadi juu ya ukarabati wa kituo hicho lakini hadi leo bado ahadi hiyo haijatekelezwa  na wananchi bado wanapata usumbufu  hususani wanawake ,watoto na watu wazima.

Mhe. Jaku ameiomba Serikali   kwavile kituo hicho kipo chini ya halmashauri  ya Wilaya ya kusini  baada ya ugatuzi  basi ni vyema  hatua za haraka zikachukuliwa  ili kukikarabati kituo hicho.

Kwaupande wake Naibu Waziri wa afya Harusi Suleiman amekiri kuchelewa  kwa ukarabati wa kituo hicho na  kuahidi  kuchukuwa hatua za haraka   kufanyiwa matengenezo ili  kuwaondolea wananchi wa maeneo hayo usumbufu.

Amesema  kupitia mpango wa mwaka 2018  halmashauri ya Wilaya ya kusini Unguja imetenga  Shillingi Million  Ishirini  kwa ajli ya matengenezo ya kituo hicho na  kazi hiyo  inatarajiwa  kufanyika katika robo ya pili ya bajetoi ya mwaka 2018/2019.

Amina Omar