Zaidi ya shillingi Millioni Mia sita zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Wete-Gando kisiwani Pemba ili kuwaondoshea usumbufu wanaoupata wananchi wakati wa safarii.

Akijibu swali la Mwakailishi wa Jimbo la Mfenesini Machano Othman Saidi katika mkutao wa Baraza la Wawakikishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar alietaka kujua ni sababu zipi zilizosababisha Barabara hiyo kutojengwa.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Muhammed Ahmada amesema kabla ya kuanza kwa ujenzi huo Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Dar Al Handasah kutoka Egypt imekusudia kuufanyia utafiti udongo  wa Barabara hiyo ili kuondoa tatizo la kuharibika Mara kwa mara baada ya kutengenezwa.

Amesema ujenzi wa Barabara hiyo utaanza baada ya kutiwa saini Mkataba wa Fedha za Mkopo zitakazotumika katika Ujenzi pamoja na fedha kutoka serikalini.

Aidha ametowa wito kwa wananchi kuwa wavumili wakati serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kuimarisha miundombinu ya barabara ili kuwawezesha wananchi kuendelea na shughuli za Maendeleo.