Serekali ya Mkoa wa Kusini Unguja imesitisha  shughuli zote za matumizi ya ardhi eneo la Dunga kiembeni  wilaya ya kati mkoa wa kusini unguja 


Kauli hiyo imekuja mara baada  ya mlalamikaji Ameir Hassan Ameir ambaye mkulima aliyengolewa miti yake ya  mnazi inayokadiriwa kukatwa  zaidi  ya mia moja.


Sheha wa shehia hiyo Abedi Hassan Abdalla amesema ni kweli upo mzozo huo wa ardhi katika eneo hilo na hatimae kung’olewa kwa mnazi hiyo zaidi ya mia moja iliyopandwa  .

Akizungumza na katika ziara Mkuu wa mkoa wa kusini unguja Hassan Khatibu Hassan amesema kuwa eneo hilo kwa sasa litakuwa chini ya serekali na kuamua kusitisha shughuli zote za eneo hilo na pia watachukua hatua za kisheria.

Nae Mkuu wa wilaya ya kati   bi Hamida Mussa Khamis   amesema kuna mzozo kati ya Abdalla Rashid pamoja na wanajeshi ambao walikuwa wakilima eneo hilo na pia upimaji wa waramani iliyopo sheha haelewi eneo hilo.

Serekali ya mkoa inajitahidi kukabaliana na changamoto za ardhi zinazofika ndani ya mkoa na halmashauri na kuwataka wananchi kuripoti chanagmoto zao na pia kuiunga mkono juhudi za serekali zilizopo chini Dk. Ali Muhammed Shein  kushughulikia changamoto za ardhi na kuzipatia ufumbuzi.

Na: Rauhiya  Mussa   Shaaban