Katika kuendeleza mapambano dhadi ya ugojwa wa CORONA Serikali ya Tanzania imetoa vitabu vya kwanzia msingi hadi sekondari kwa njia ya mtandao ili kuwaaidia wanafunzi katika kipindi hichi likizo

Akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na kusema, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako huko bungeni Dodoma amesema.

“Tunajua kuwa  wanafunzi kwa sasa wapo nyumbani na wanahitaji kuendelea kupata elimu hata wakiwa nyumbani, tunayohuduma ya maktaba inayotolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania ambayo kiutaratibu ili uweze kupata vitabu ilipaswa mtu kulipa, sasa serikali inatoa huduma ya upatikanaji wa vitabu vyote kuanzia shule za msingi na sekondari bila malipo yeyote,”alisema waziri huyo.

Aidha wametakiwa kutumia muda wao wa likizo hii kusoma vitabu ambavyo Serikali imewapa bila gharama yeyote badala ya kuzurura mitaani na kujiweka  kwenye hatari ya kupata maambukizi ya Corona.