Ibrahim Mohamed kibavu mwenye umri wa miaka 31 mzaramo wa paje, amemshambulia na Peris Yohana said mwenye umri wa miaka 20 Mnyiramba wa paje ambae ni mpenzi wake kwa kumchoma na kisu kifuani, chini ya ziwa la kushoto na kumsababishia maumivu makali pamoja na kupoteza damu nyingi ambapo chanzo cha ugomvi huo unadaiwa na wivu wa mapenzi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema mnamo tarehe 24/06/20 saa 2:30 usiku wawili hao walikuwa wakigombona na ndipo mtuhumiwa alimchoma kisu mpenzi wake na kumsababishia maumivu makali mwilini, mtakiwa huyo amekamwatwa na uchunguza wa shauri hilo unaendela.

Aidha kamanda Suleiman ametoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi mwao na badala yake kuyapeleka matatizo yao kwa familia au vyombo vya sheria