Shamra shamra za kinyang’anyiro cha Urais chazagaa skuli ya AL HISAN Unguja

Wanafuzi Skuli ya Secondary Al hisan iliyopo mwanakwerekwe  Jitimai ya Zamani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Kinyanganyiro cha uchaguzi wa ngazi ya urais na Makamo wa Raisi wa Skuli ya AL HISAN GIRLS SECONDARY SCHOOL iliyopo mwanakwerekwe  Jitimai ya Zamani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Jumla ya wagombea wanne wa ngazi  tofauti ngazi ya Rais inajumla ya wagombea wawili Mastura Saidi Khamisi kidato cha Tano Sanaa(ART), mwengine ni Weje Maalim Saleh ,kidato cha Tano sayansi.

Kwa upande wa makamo wa Rais jumla ya wagombea wawili Khairati Shaabani Chumu kidato cha Tatu (Sayansi) na Khadija Ali Nassor kidato cha kwanza.

Akizugumza na Zanzibar24 mgombea wa Uraisi Mastura Saidi Khamisi amesema endapo atapochaguliwa kuongoza skuli hiyo atahakikisha skuli yake inakuwa juu  kimasomo na ikiwezekana kuingia kwenye kumi (10) bora Tanzania, licha ya kushika nafasi mwanzo kwa somo la Kiarabu Kidato cha Sita mwaka uliopita.

Wagombea ngazi ya Urais pamoja na ngazi ya umakamo Skuli ya Al hisan iliyopo mwanakwerekwe  Jitimai ya Zamani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Amesema ataanzisha mfumo wa kila mwanafuzi kupewa zawadi ya mwanafunzi bora wa kila somo,pia amesema atashirikiana na uongozi wa skuli kuboresha mahusiano na skuli nyengine kubwa ili kuongeza ufaulu shuleni pao.

Kwa upande wake mgombea wa Uraisi Weje Maalim Saleh amesema kwenye ahadi zake atahakikisha kuimarisha michezo ndani ya skuli ya Al Hisaan licha ya skuli hiyo kuwa ya wanawake watupu, atandaa utaratibu wa kuwahamasisha wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika kesho majira ya saa mbili za Asubuhi ndani ya Skuli hiyo na utasimamiwa na wajumbe wafuatao wa tume ya uchaguzi.

Sharifa Rashidi    –     Mwenyekiti.

Zuwena Abeid      –     mjumbe.

Ziada Mussa           –    Katibu.

Zulfa Omar Khalfan  –    Mjumbe.

Maryam Hassan    –       Mjumbe.

Jumla ya wanafunzi 410 wanatarajiwa kushiriki  kwenye uchaguzi huu wa mwaka 2018 wa skuli ya Al Hisan Girls  .