Wazazi na walezi wametakiwa kuwa na tabia ya  kuwaangalia watoto wao mara kwa mara wanapocheza  na kutowaachia kuangalia tv wakiwa pekeyao ili kuwaokoa na majanga yaayojitokeza

Akitoa wito huo  mara baada ya kutokea tukio la kifo cha mtoto Lukman Salim Mohammed mwenye umri wa miaka 10 ambae amekutwa ameshafariki dunia huku mwili ukining’inia wakati akiigiza kujinyonga kama alivyoona kwenye tv, sheha wa shehia ya Wawi Mjengo wa Banda ndugu Rashid Issa Juma wakati akizungumza na zanzibar24 kwa njia ya Simu amesema

watoto hupendelea kujaribi vitu wanapoona bila kufikiria madhara ya baadae hivyo kuwataka wazizi wapendelee kuwaachia watoto kuangalia tv bila uangalizi wa mtu mzima

Aidha sheha huyo amewataka wanafamilia hao kuwa na moyo wa  subira katika kipindi hichi kigumu cha msiba