Mjumbe wa Baraza la Maulamaa Zanzibar Mkoa wa Kusini Pemba Sheikh Ali Abdala Awess amewataka Masheikh na Wazazi  kuelimisha Vijana  suala la Ndoa ili kunusuru Wimbi la kuvunjika ndoa nyingi  mapema.

Shikh Awess  ameyasema hayo  Kwenyeskiti wa Ijumaa  Mtambile alipokua akizungumza na Waislam mara baada ya Swala ya Ijumaa.

Amesema kwa sasa ndoa nyingi za vijana zinavunjika mapema na kusababisha idadi kubwa ya Wajane na watoto wasio na malezi bora kutokana na kukosekana kwa Taaluma ya ndoa.

Hata hivyo amesema kuwa taaluma  ya Mapema  kwa Wanandoa  ni njia pekee itakayowafanya  waishi ndani ya Ndoa yao kwa mafanikio zaidi.

Wakati huo huo mjumbe  huyo  wa  Baraza la maulamaa ameelezea  kusikitishwa  na tabia   iliyojitokeza  kwa baadhi  ya misikiti kuisali Sala  ya Ijumaa nje ya wakati  wake.

Amesema imejitokeza baadhi ya miskiti  inasali  Sala  hiyo  nyakati  za  saa tano  kitendo ambacho hakifai na kiachwe ili kulinda nyakati  za sala pamoja na kutodharau sheria za dini ya kiislam.