Sherehe za Mapinduzi: Ulinzi waimarishwa Pemba

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Kusini Pemba Wamejipanga kuweka Ulinzi wa kutosha katika mkoa huo kwa lengo la kuhakikisha usalama wa kutosha kwa Viongozi na Wageni wote Waliofika mkoani humo Kwa Ajili Ya Sherehe Za Mapinduzi Ya Zanzibar Yatakayofanyika Januari 12 Mwaka Huu Huko Kisiwani Pemba.

Hayo yamebainishwa na Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Kusini Pemba Kamishna Msaidizi Muandamizi Hassan Nassir Ali.

Amesema Jeshi la polisi linaendelea na Doria Kuweka Ulinzi kulingana na Vifaa MbaliMbali Walivyonavyo Ambavyo Vinawapa Nguvu Ya Kuweka Ulinzi Na Usalama.

Katika harakati hizo za Sherehe za mapinduzi Zinazotarajiwa Kufanyika Uwanja Wa Gombani Pemba Kamanda Naasir Amewataka Wananchi Kutoa Ushirikiano Na Jeshi La Polisi Ilikutambua Usalama Wao Na Kuacha Kuwakumbatia Wahalifu wanaoweza kuzichafua Sherehe Hizo Za Miaka 55 Ya Mapinduzi Ya Zanzibar.

Rauhiya  Mussa Shaaban