Mwanamuziki Shilole, ameamka na kuibua zogo katikati ya kikao cha wawekezaji wa kampuni ya ‘SwahiliFlix’ ambao wamekuja kuwekeza kwenye filamu baada ya mzungumzaji wa kikao hicho kuonekana akitumia zaidi lugha ya Kingereza ambayo msanii huyo amedai wasanii wengi hawaifahamu.