Shilole avunja ndoa ya Tanasha ampa ushauri Diamond

Muigizaji wa zamani ambae kwasasa ni msanii wa Bongo Fleva, Shilole amemshauri Diamond Platnumz kumuoa aliyekuwa mpenzi wake na mzazi mwenzie, Zari The Bosslady.

Shilole akizungumza na Wasafi TV amesema kuwa ukiachana na Zari haoni msichana mwingine wa kumfaa muimbaji huyo pendwa kutoka WCB.

“Nitafurahi sana Diamond akioa ila katika kuoa kwake ajaribu kurudisha kumbukumbu nyuma, amuoe Zari hata kama atamuoa mwanamke mwingine sijiu nani anaweza kumfaa,” amesema Shilole.

Ni takribani mwaka mmoja tangu Diamond kuachana na Zari na kuanzisha mahusiano mapya na mrembo Tanasha kutoka nchini Kenya.

Hivi karibuni Diamond Platnumz alikaririwa na kituo hicho cha runinga akieleza kuwa ndoa yake aliyopanga kuifunga mwezi wa pili mwaka huu ameisogeza mbele.