Shirika la Ndege la SWISS International Airlines ambalo linamilikiwa na Shirika la Ndege la Lufthansa la Ujerumani, limesimamisha safari za ndege zake zote aina ya Airbus A220 kutokana na matatizo ya Injini zake

Ndege hizo ambazo hutumia injini aina ya PW 1500G zinazotengenezwa na Kampuni ya Pratt & Whitney ya Canada zimelazimika kukaguliwa ili kuhakiki usalama wake.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA) ilitoa muongozo kwamba injini zote za A220 ambazo ni Pratt & Whitney zinatakiwa kufanyiwa ukaguzi zaidi wa kiusalama kunatokana na matatizo ya kiufundi ya mara kwa mara ya injini hizo

Mnamo Julai 25, vipande vya injini ya A220 vilikatikakatika na kuanguka katika Anga la Paris wakati ndege hiyo ikiwa safarini kutokea Geneva kwenda London. Tukio kama hilo linaripotiwa kutokea tena Septemba 16