Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimepiga marufuku uingizaji, usambazaji na uuzaji wa bidhaa za siagi, zilizotengenezwa kwa karanga kutoka Kenya baada ya kubainika kuwa na vimelea hatarishi kwa afya za walaji

Kwa mujibu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), bidhaa hizo zimezuiwa kuingia Tanzania kutoka Kenya ili kulinda afya za Watanzania, kutokana na uchunguzi uliofanywa na Shirika la Viwango la Kenya (KBS) kubaini zina sumu kuvu, inayoweza kusababisha ugonjwa wa saratani kwa binadamu

Nchi za Rwanda na Uganda, pia zimepiga marufuku bidhaa hizo kuingizwa na kutumiwa katika nchi hizo kutokana na athari zake

Bidhaa zilizopigwa marufuku ni Truenutz iliyokuwa ikizalishwa na Truenutz Kenya, Fressy iliyokuwa ikizalishwa na Fressy Food Company Limited, Supa Meal iliyokuwa ikizalishwa na Supacosm Products Limited

Nyingine ni Nuteez iliyokuwa ikizalishwa na Jetlak Foods Limited, Sue’s Naturals iliyokuwa ikizalishwa na Nature’s Way Health, Zesta iliyokuwa ikizalishwa na Trufoods Limited na Nutty