Sijawahi kufikiria kufunga ndoa na Iyobo -Aunt Ezekiel

MUIGIZAJI wa  filamu Bongo, Aunt Ezekiel, ambaye pia ni mzazi mwenzie na dansa maarufu wa Wasafi Classic Baby (WCB), Moses Iyobo, amesema kuwa hana mpango wa kufunga ndoa na dansa huyo japokuwa wameshakaa wote zaidi ya miaka mitatu kwani kikubwa wanachokiangalia ni kulea mtoto wao Cookie.

Akizungumza na Amani, Aunt alisema kuwa siyo kwamba mtu akifunga ndoa ndiyo anaweza kuishi vizuri na mwanaume wake, bali ni kwamba anachojua kuishi vizuri ni sifa moja kubwa ya kuendelea kuwa pamoja ni kupeana heshima na kila mmoja kutambua anachokifanya.

“Mimi sitaki hata kukuficha wala sijawahi kufikiria kufunga ndoa na Iyobo leo wala kesho kikubwa tunaishi vizuri na tunalea mtoto wetu ipasavyo hilo ndilo ninalolitaka na si vinginevyo kwani kuolewa siyo ishu kikubwa malezi ya mtoto tu,” alisema Aunt.