Waziri wa habari utalii na mambo ya kale Mh. Mahmoud Thabit Kombo amevitaka vyombo vya habari kuifuata misingi ya sheria ya nchi ili kujenga taifa endelevu na lenye amani.

Ametoa kauli hiyo wakati akisoma hutba yake katika maadhimisho ya siku ya radio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Zanzibar beach resort huko Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar

Amesema vyombo vya habari  ndio vyenye guvu na muhimu  kwani husaidia kufikisha taarifa kwa urahisi katika maeneo mbalimbali ikiwemo vijijini hivyo ni vyema kuilinda misingi na sheria ili kuenendeleza amani na utulivu wa nchi na kuepusha migogoro katika jamii

Nae Mwenyekiti wa bodi ya mtandao wa TADIO Prosper Kwigize Amevitaka vyombo vya habari kutengeneza vipindi mbalimbali ambavyo vitakavyo saidia kuondosha changamoto na kuleta maendeleo

Siku ya Radio duniani huadhimishwa kila ifikapo febuary 13 ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Radio na ujumuishaji” na kwamara ya kwanza siki hii imeadhimishwa visiwani Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali