Uongozi wa klabu ya Simba umewaonya baadhi ya watu au makundi ya watu ambao wamekuwa wakiingia makubaliano au mikataba na taasisi au kampuni nyingine, wakijiwasilisha kama wafanyakazi au wawakilishi wa kampuni ya klabu ya Simba.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingiza katika taarifa yake kwa Umma, amesema klabu hiyo haijatoa mamlaka kwa mtu yeyote au kikundi cha watu kuingia makubaliano au kusaini mikataba kwa niaba ya Simba.

Aidha Simba imekemea vikali vitendo vya namna hiyo na kuwaomba Wananchi kutoa taarifa za watu wa namna hii katika ofisi ya Mtendaji Mkuu wa klabu.