Simu za kukunja mfano wa waleti zazinduliwa nchini China

Marekani imeweka rekodi kwakuwa ya kwanza kuzindua simu ya ambayo unaweza kukunjwa ndani ya Kampuni ya kiteknolojia yenye makao yake California.

Kampuni hiyo imeanza kuuza simu hiyo janja nchini China tarehe 31 ya mwezi Oktoba baada ya kuzinduliwa kwake.

Royole Corporations imezindua FlexiPai katika hafla ya kufana mjini Beijing China.

Gharama yake inakadiriwa kuwa Yuan 8,999 (dola 1,290), RAM GB 6 Snapdragon 8-series. Hata hivyo Royole FlexPai huwenda ikaanza kupata ushindani baada ya Samsung nao kutarajia kutoa toleo lake jipya juma lijalo huku LG na Huawei nao wameripotiwa kufanya mageuzi makubwa ya simu janja za mkononi ‘Smartphone’. FlexPai imebezi zaidi katika simu aina ya ‘tablet-phone’ ina nchi 7.8 na features ratio 4:3.