Sita wakamatwa na Dawa za kulevya Zanzibar, haya hapa majina yao na wanapoishi

Watu sita wanashikiliwa na Polisi kwa madai ya kukutwa na dawa za kulevya aina tofauti na viwango tofauti katika maeneo mbali mbali Ya mji wa Zanzibar.

Akithibitisha kukamatwa kwa watu hao Mkuu wa Kitengo Cha Polisi dawa za kulevya Makao Makuu Ya Polisi Zanzibar SSP Omari Khamis amesema wanaendelea na mapambano dhidi Ya dawa za kulevya ambapo kwa mwezi Octoba mwaka huu tarehe 27 na 30 wamewakamata watu sita wakiwa na bangi, vifuko vya unga na sampuli Ya vijiwa aina tofauti na viwango tofauti katika maeneo tofauti Ya mji wa Zanzibar.

Amewataja watu hao kuwa ni Hamadi Suleiman Abdallah (40) Makadara akiwa na unga sampuli ya vijiwe 3, Joseph Maiko Joseph (28) Kisauni akiwa na vifurushi vya Bangi 2, Ali Juma Muhsini (30) Kijichi akiwa na unga vijiwe 16, Suleiman Ramadhan Suleiman (24) Kilimani akiwa na vifurushi vya bangi 8 ,Harithi Abdulhamid Abdallah (19) Kinuni akiwa na Nyongo 15 za bangi pamoja na Mrisho Rajabu Iddi Fuon Maharibiko akiwa na vifuko 2 vya unga wa Kokeni.

Ameongeza kusema kuwa bado biashara hizi za dawa za kulevya zinaendelea katika mitaa yetu ingawa zinafanyika katika hali ya kificho ambazo ndani yake zinaleta athari kubwa katika jamii zetu.

Aidha SSP Omari ameitaka jamiii kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pamoja na kitengo cha kupambana na dawa za kulevya ili kuweza kutokomeza janga hilo ambalo linaleta athari kubwa kwa vizazi vyetu na pia kupiga vita dawa hizo za kulevya.

Rauhiya Mussa Shaaban.