Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa kiapo mbele kwa wanafunzi waliofaulu  kidato cha sita kwa ufaulu mzuri na kutoa udhamini wa masomo ya elimu ya juu ndani na nje ya nchi ya Zanzibar.

Akizugumza na Wanafunzi waliomaliza kidato cha Sita na kutarajiwa kujiunga na elimu ya juu ndani na nje ya Zanzibar, Waziri wa elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Riziki Pembe Juma amesema kuwa Serikali imetoa kipaumbele kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na kuelekea elimu ya juu ndani na nje ya Zanzibar ili kuweza kuweza kujinasua katika soko la ajira kwakupewa  kipaumbele katika suala la ajira .

Hata hivyo amewataka wanafunzi hao kusoma masomo ya sayansi na kusoma kozi ambazo Serikali inazitambua kwa kua nchi inahitaji wataalamu wakufanya kazi kwakuwa wataalamu ni wachache katika nyanja tofauti.

“Mwaka huu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa nafasi 30 za udhamini wa vyuo tofauti kwa wanafunzi waliofanya vizur ukilinganisha  na mwaka uliopita tulitoa nafasi 20 tu” Alisema Riziki Pembe.

Kwa upande mwengine amewashauri kujitambua na  kutumia vizuri nafasi ambazo wamepatiwa ili kujua kuwa wataporudi kuna familia zao ambazo zinawategemea katika maisha.

Kwa upande wake kamishina kutoka Tume ya mipango Zanzibar Bi Salama Makame ametilia mkazo suala la wanafunzi kuchagua kozi ambazo serikali inazitambua, Vile vile  alivitaja vipao mbele tofauti  vya serekali alitaja vipengele ya kozi zilizopewa kipaombele.

“Upande wa elimu ni sayansi na mathematics,geography,usimamizi wa maswala ya sayansi “ Alimazia kwa kuzitaja

Nae mtoa  mada ambae ni muwezeshaji na mtumishi wizara ya afya Zanzibar Ramadhan Khamis amesema kuwa  wizara ya afya sera yake kutoa huduma ya afya iliyo bora, na ametilia mkazo kwa kusema fani ya afya inahitaji watu waliosomea vizur, kwakua kwa kila mwaka idadi ya watu inakuwa na maradhi yanaongezeka kwaiyo na wataalam wanahiji kuengezeka ili tuweze kuwepo mbali katika suala la afya.

Kwaupande wa wanafunzi ambao waliomaliza kidato cha sita wamesema kuwa  wanafurahia kuwepo kwenye mafunzo hayo,   yamezungumziwa masuala ya kuchagua kozi zilizo bora atapokwenda chuoni, pamoja na kufurahiswa na kutolewa nafasi 30 za kusoma nje na Raisi wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein nakuomba kuongezeka kwa mwaka ujao.

Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa Skuli ya Haile Selasi na kuhudhuriwa na wanafunzi waliomaliza kidato cha sita wenye sifa ya kwenda kuanza kusoma chuo kikuu na pamoja na wadau mbalimbali katika sekta ya elimu.