Kamati ya Fedha , Biashara na kilimo ya baraza la Wawakilishi imeitaka Wizara Fedha Mipango kudhibiti tatizo la Uvujaji wa mapato ya Serikali yanayotokana ana Vyanzo vya mapato ya Ndani.

Akiwasilisha Ripoti ya kamati ya Fedha ,Biashara na kilimo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Yussuf Hassan Iddi amesema bado kuna baadhi ya maeneo ya ukusanyaji wa Mapato hayafikiwi jambo ambalo linachangia upotevu wa fedha za serikali.

Amesema Wizara hiyo itakapofanya kazi kwa kufuata sheria itaiwezesha serikali kufikia malengo waliyakusudia katika ukusanyaji wa mapato ili kuimarisha huduma za maendeleo kwa wananchi.

 Pia, amesema kua makusanyo ya vyanzo vya mapato ya ndani yameimarika hadi kufikia asilimia 20 jambo ambalo linaleta matumaini makubwa ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza azma yake ya kufikia Uchumi wa Viwanda.

Mwenyekiti huyo ametowa wito kwa watendaji wa Wizara hiyo kuachana na muhali katika kutelekeleza majukumu yao pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaokwepa kulipa kodi ili kuimarisha Uchumi wa Nchi.

Wakati huo huo kamati hiyo imeitaka Wizara ya kilimo Maliasili ,Mifugo na Uvuvi kuwa na Utaratibu wa kusomesha wafanya kazi wao ili kuengeza wataalamu katika Wizara hiyo.

Amesema Wananchi wamekuwa na mahitaji makubwa kwa wizara hiyo laikini baadhi yao wanashindwa kutatuliwa matatizo yao kutokana na uhaba wa wataalamu katika wizara hiyo.

Aidha ametowa wito kwa wizara kuendelea kuwahamasisha wakulima kulima kilimo cha Biashara na Chakula ili kupunguza kasi za kuagizia vyakula kutoka nnje ya Zanzibar.

Na;Fat-hiya Shehe Zanzibar24.