Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar imewataka wananchi wanaojishuhulisha na kazi za uvuvi  kuwa  wavumilivu kwani Serikali ipo kwenye  harakati za kuhakikisha sheria ya uvuvi bahari kuu inaleta manufaa pande zote mbili visiwani zanzibar na Tanzania bara.

Akijibu suali lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesi Machano Othman Said  kuhusu  Serikali ya SMZ  imechukua hatua gani  juu ya Sheria ya uvuvi bahari kuu  ili iweze kutumika pande mbili  Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dk. Makame Ali Ussi amesema harakati bado zinaendelea za kuifanyia kazi sheria hiyo ili iweze kutumika zanzibar.

Amesema licha ya SMZ kuendelea na harakati hizo za kufatilia sheria  lakini Zanzibar inapata mgao wake wa fedha kutokana na uvuvi wa bahari kuu ambapo mgao huo unagawiwa katika sehemu tatu  asilimia 50 inabakia ndani ya Mamlaka ya uvuvi wa bahari kuu na asilimia inagaiwa pande mbili ambapo zanzibar na Tanzania bara.

Amesema pia  bado wavuvi wanafursa ya kuvua katika bahari ya ndani na ya kati lakini watakapo kwenda kuvua bahari kuu lazima hapo wafuate sheria za  Tanzania bara na itawabidi wakate lessen ili kuvua bahari kuu na wanapovua za ndani pia wakate lessen ya SMZ.

Amina Omar