SMZ  imesema  inaendelea na taratibu za kutangaza tenda kwa ajili ya ukaguzi wa magari  katika nchi nne ambapo  nyaraka za tenda hizo  zimeshataarishwa.

Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali amesema miongoni mwa nchi  ambazo wanatafutwa wakala ili kupewa tenda kwa ajili ya ukaguzi wa magari ni Japani,Hongkong,Singapore na Uingereza.

Aidha amesema hivi sasa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikifaidika na asilimia 30  ya makusanyo  ya kodi  kutoka kwa wakala wa kuchunguza  bidhaa  zinazoingia  nchini mpaka pale ZBS itakapokuwa na uwezo  wa maabara  ambapo watapima  mara tu bidhaa zitakapoingia nchnini Zanzibar.