Serikali ya mapinduzi zanzibar, imepiga marufuku wanasiasa kutumia nyumba za ibada kwa shughuli za kisiasa hapa nchini.

Akitoa tamko la serikali waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais, mhe, Mohammed Aboud Mohammed amesema kwamba viongozi wa dini na kamati zao katika nyumba za ibada watakaoruhusu wanasiasa kuendesha shughuli hizo watawajibika kwa mujibu wa sheria za nchi.

Amesema kwamba hivi karibuni katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa mjini magharibi unguja kumetokea tabia kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa kupita na kutoa hotuba za kisiasa katika nyumba hizo.