Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inaendelea na Mpango wake wa Ujenzi wa kiwanda cha kusindika mwani pamoja na kufanya utafiti wa mazao na masoko ya mwani zanizbar.

Akijibu swali katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Chukwani,Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda  Hassan Hafidh amesema mpaka sasa serikali imetenga shillingi Millioni 450 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Amesema utekelezaji wa mradi huo baada ya kukamilika utaweza kuwasaidia wakulima kunufaika na zao hilo pamoja na kuweza kujiajiri kupitia Rasilimali za baharini.

Amesema ujenzi wa kiwanda hicho utatekelezwa na Serikali ya Zanzibar  pamoja na wadau wa maendeleo kwa lengo la kuwasaidia wakulima kupata masoko ya uhakika pamoja na kuzalisha bidhaa za mwani zinatakazo endana na soko la dunia.Naibu Hafidh amesema tayari serikali inaendelea na mazungumzo na wadao hao wa maendeleo ili kutekeleza mradi huo kwa wakati ili uweze kuwanufaisha wananchi.