Snura apata ajali ya gari akiwa na mpenzi wake

Msanii wa muziki Bongo, Snura Mushi amepata ajali ya gari akiwa na mtu wake wakaribu anayedaiwa kuwa mpenzi wake pamoja na madensa wake wawili waliyokuwa pamoja kwenye usafiri huo wakielekea mkoani Lindi kwaajili ya kufanya shoo.

Kwamujibu wa mtu wake wakaribu anayedaiwa kuwa mpenzi wake, Minu Calypto ameandika ujumbe kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram kuwa wamepata ajali hapo jana Agosti 9, 2018 majira ya saa nne za usiku.

“Jana mida ya saa nne usiku tulipata ajali mi na @snuramushi na ma-dancer wetu wawili pamoja na dereva.. Gari ilipinduka ila tunashkuru mungu tuko salama.. #WeGood”