Mratibu wa Mradi wa Malezi mbadala SOS Bi Nnyezuma Simai Issa amewataka waandishi wa Habari kutumia kalamu zao kwa lengo la kuelimisha jamii pamoja na kuihamasisha katika ngazi tofauti za kimaisha.

Ameyasema hayo katika kikao cha kujadili mambo tofauti yanayohusika na mradi wa Malezi mbadala unaotendeka katika kisiwa kidogo kilichopo tumbatu Kaskazini Unguja huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema katika Mradi huo wamefanikiwa kutoa elimu kwa jamii pamoja na kutoa misaada mbalil mbali katika familia husika na hatimaye waliopo katika mradihuo wametoa shukrani kubwa kuhusiana na mradi huo.

Nae Meneja Mradi kutoka Muzdalifa Mohammed Ali Muhammed amesema kuwa jamii ya waliopata bahati ya kupata mradi huo bado hawajaelimika katika suala zima la kadi aza Afya kwani wengi wao hawazitumii kadi hizo hatimaye kutoa pesa zao mikononi kwa ajili ya matibabu.

“Nahisi wanaona uzito katika kutumia au vipi maana kuna baadhi hawana uelewa mtu tunamwambia tuoneshe kadi yako apo alipoieka ashaisahau

“Si maana aende mkokotoni kupata huduma tu ata hospitali kuu ya mnazi mmoja inamruhusu kadi yake kupata huduma”amsema Muhammed

Kwaupande wake Afsa Ustawi  Jamii Mkoa wa Kaskazini ‘A’  Makame Makame Haji amesema kuwepo kwa changamoto ya huduma ya Afya kwa wajawazito wakati wa kujifungua suala hilo watalifanyia utaratibu kwa kulifikisha mikononi mwa Serikali ili kupatiwa ufumbuzi zaidi.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Maafsa wa Mikoa tofauti  kisiwani Unguja kwa lengo la kutoa uthibitisho wa halihalisi ya Maendeleo na changamoto zilizopo ndani ya kazi zao zinazohusiana na mradi huo.

Mradi wa Malezi Mbadala umeanza  mwaka 2017 na unatarajiwa  kumaliza mwaka Dicemba 31 -2019 ambapo Tumbatu ni kisiwa kilichofanikiwa kupata bahati ya kuelimishwa pamoja na kupewa huduma ya malezi mbadala ili kuimarisha malezi ya watoto waliopoteza malezi nawengine walio katika hatari ya kupoteza malezi bora.

Na: Tatu Juma.