Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kusini Unguja (SOURFA) kimekutana na Vyama vya Soka vya Wilaya ya Kusini Unguja na Wilaya ya Kati kwaajili ya kutambuwana na kupanga maandalizi juu uteuzi wa Wachezaji Vijana Chini ya umri wa miaka 15 na 17 ambao wanatakiwa kwenda kucheza Mashindano ya Taifa ya Vijana jijini Dar es salam mwezi June mwaka huu.

Katika kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa SOURFA Shauri Hassan Jaku kimewatangaza makocha wa kombain ya mkoa wa Kusini kuwa ni Ali Khalid Omar, Yussuf Khamis, Kijo Nadir Nyoni na Mohd Iddi (Udero) ambao watazisimamia timu za mkoa huo chini ya miaka 15 na chini ya miaka 17.

Akizungumza kwa niaba ya ZFA Wilaya ya Kusini na Wilaya ya Kati Ahmed Ussi amesema wao kama ZFA Wilaya wamefarijika kuona FA Mkoa wa Kusini kukaa nao pamoja kwa lengo la kujenga maendeleo bora ya soka ndani ya mkoa huo.

Wakati huo huo Kamati Tendaji ya Chama cha Soka Mkoa wa Kusini Unguja wamemchagua Makamo Mwenyekiti wao Abubakar Khatib Kisandu kuwa msemaji mkuu wa chama hicho kama hapa katibu wa FA Mkoa huo Masoud Ali Dau.

Kwa upande wake Abubakar Khatib Kisandu ameipongeza kamati tendaji hiyo kwa kumchagua lakini amesema SOURFA kwa pamoja bado wana kazi nzito huku akisisitiza mashirikiano.