Steve Nyerere aibuka msiba wa Producer Pancho Latino

Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania ambaye pia ni mratibu wa shughuli za misiba kwa wasanii Steve Nyerere amefunguka na kuwajibu wanaombeza na kumtukana anapojitoa mstari wa mbele kuposti taarifa za misiba au matatizo ya kijamii adai kamwe hatorudi nyuma

Steve nyerere ametuma ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa instagram Jana Oktoba 9 Kufuatia kifo cha  Producer  Pancho Latino kutoka studio za B-Hitz ambaye amefariki jana jioni kwa ajali ya maji.

Steve Nyerere amekuwa mstari wa mbele kuwaunganisha wasanii hasa katika kipindi cha misiba au matatizo yanayowatokea wasanii wenzao.