Mwanasheria maarufu nchini Tanzania Alberto Msando ambaye ndiye aliyejitolea kuwatetea wasanii waliotajwa na Mkuu wa Dar es Salaam kuwa wanatumia madawa ya kulevya.

Mapema leo February 14, Mwanasheria Msando alifunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa hatowatetea wanaohusika na kuingiza, kusambaza na kuuza madawa ya kulevya.

Kutokana na kauli hiyo Mkali wa wimbo wa Dume Suruali ambaye pia ni rafiki wa mwanasheria huyo alimtupia swali mwanasheria huyo: “Kwa hiyo Mwanasheria Msomi,mtu akikamatwa na ganja yake moja utamtetea ama asikujue?we(me and @hermyb ) are asking for a friend ?”

Mwanasheria huyo aliandika hivi:

Vita dhidi ya Madawa ya Kulevya sio ya Dar Es Salaam peke yake tena. Ni ya nchi nzima. Jambo moja zuri baada ya Mh. Makonda kuamua kulivalia njuga kwa Dar peke yake Kamishna ameteuliwa. Na Raisi ameifukua sheria ambayo amesema ‘ilifichwa’. Kama vita hii isingeanzishwa sheria hii ingeendelea kubaki kabatini. Ukweli ni kwamba watu wengi hawana raha kwa sasa. Wale wote ambao wamekuwa wanajihusisha na kutumia sasa hivi roho juu. Hii angalau ni hatua. SASA ni muda wa kushirikiana na mamlaka husika kupambana na madawa ya kulevya. Kamishna amesema wazi kwamba hakuna jiwe ambalo litaacha kugeuzwa. Na ameahidi kufuata sheria na hakuna atakayeonewa. Yale malalamiko ya sheria kutokufuatwa na uonevu yamepatiwa majibu. Binafsi namsupport Kamishna katika jukumu lake hili. Nitawatetea wale tu ambao watakuwa wanaonewa na walioathirika na madawa. WANAOHUSIKA NA KUINGIZA, KUSAMBAZA na KUUZA MADAWA YA KULEVYA SITAWATETEA. Madhara ya madawa ya kulevya ni makubwa mno. Mshauri rafiki yako au mtu wako wa karibu asije kuthubutu kutumia na kama anatumia aache. Kuna watu hawajui kama BANGI na MIRUNGI ni dawa za kulevya. Acheni. Watumiaji wa BANGI wako wengi. Na wengi marafiki zetu. Siku ukijikuta lock up na mbele ya Mahakama usishangae!! #SayNoToDrugs #LetsJoin #LetsSupport#CentresVersusPrisons