TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


TAMWA yashukuru kukamatwa kwa mdaiwa uuwaji

Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA,
ZNZ), kinawashukuru jamii/wananchi kwa kutoa mashirikiano kwa jeshi la polisikufanikisha kukamatwa kwa Haji Jaha Issa (25) mkaazi wa eneo la Paje KusiniUnguja ambaye anatuhumiwa kuhusika na kifo cha Hajra Abdallah Abdallah (21).


Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini, Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema jeshi la polishi limeweza kumkamata Haji Jaha siku ya Agosti 1, 2020 katika kijiji cha Msisi wilaya ya Handeni Mkaoni Tanga.


Kamanda Suleiman amesema raia wema ndio waliyotoa taarifa hizo baada ya mtuhumiwa kuwaomba hifadhi ili andelee kujificha lakini jeshi la polisi baada ya kupata taarifa hizo lilifika eneo hilo na kumkata kumrudisha Zanzibar Agosti 4, 2020 pamoja kumfikisha Mahakama kuu ya Vuga, Zanzibar Agosti 28,2020ambapo kesi yake itaendelea tena Octoba 9, 2020.


“Kazi ya kutafuta na kukamata inakua nyepesi kwa jeshi la polisi pale ambapo jamii wanatoa mashirikiano, raia wema walitupa taarifa kama mtuhumiwa yuko Tanga kijijini eneo la Msisi Handeni, anaomba hifadhi baada ya kupata taarifa hiyo Jeshi la polisi lilimkamata mtuhumiwa kwa dakika chache tu, ” Alisema Suleiman.

Takriban ni miezi saba sasa tokea Hajra auwawe huko Paje mkoa wa Kusini, Unguja mnamo tarehe 26/2/2020 kamaa alivyoonekana majira ya saa tisa mchana.

Mama mzazi wa Hajra, Lela Leo pia amewashukuru wananchi pamoja na jeshi la polisi kwa kufanikisha kumkamata Haji amabaye anatuhumiwa kwa kifo cha mtoto wake.


Mama/ Bi Lela pia ameomba vyombo vya sheria kushughulikia vilivyo kesi hiyo ili haki ya kifo cha mwanawe iweze kupatikana.
Kutokana na hali hiyo, TAMWA ZNZ inaviomba vyombo vya kusimamia sheria kuhakikisha wanatenda haki dhidi ya tukio hilo ili kustawisha utawala wa sheria na kukomesha vitendo hivi vya kudhuru wanawake kutokana na udhaifu wao wa kimaumbile.


TAMWA ZNZ imerikodi matukio 17 ya mauaji ya wanawake Zanzibar tangu mwaka 2016 ambapo kati ya matukio hayo, ni kesi nne ikiwemo hii ya marehemu Hajra ndizo zilizofikishwa Mahakamani. Kwa taarifa ambazo TAMWA ZNZ imezipata kesi zilizosalia watuhumiwa wao bado hawajafikishwa Mahakamani kutokana na kile kinachodaiwa kutokukamilika kwa ushahidi au kutokupatikana kwa watuhumiwa.


Kesi nyengine tatu zilizofikishwa Mahakamani inawahusu Wasila Mussa (21), Samira sultan (56) na Zawadi Paulo (35) ambazo zote zinaendelea katika Mahakama Kuu ya Vuga, mkoa wa Mjini Magharibi.


Dkt. Mzuri Issa
Mkurugenzi,
TAMWA ZN