Taarifa rasmi: Hii hapa idadi na majina ya waliokufa ajali ya Ufufuma Chwaka

Watu saba akiwemo mmoja raia wa Kenya wamefariki dunia papo hapo katika ajali ya gari mbili zilizogongana huko Ufufuma kijiji cha Chwaka Wilaya ya kati ndani Ya Mkoa wa Kusini Unguja.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo la ajali Kaimu Kamanda wa Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi Khadija Haji amesema ajali hiyo iliyohusisha gari mbili moja ya Abiria ya Chwaka pamoja na basi la wafanyakazi wa hoteli (Staff Bus) wa Uroa Bay ambazo ziligongana na kusababisha vifo vya watu saba.

Watu wanne walifariki papo hapo na wengine watatu hali zao zilikuwa mbaya na kufariki dunia wakiwa hospital Ya Mnazimmoja.

Ajali hiyo ilitokea tarehe 26-10-2018 majira Ya saa 11 Jioni huko Mfufuma katika kijiji cha Chwaka.

Kamanda Khadija amesema  chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo Dereva wa gari ya basi la stuff alilewa na kwenda kuigonga gari Ya abiria ya Chwaka iliyokuwa imesimama kwa ajili Ya kupandisha mizigo na hatimae kutokea ajali hiyo Kubwa.

Aidha Kamanda Khadija amewataja marehemu hao kuwa Mtoto Miraji Khamis, Magret Joseph, Kissa Yessaya, Neema John, Justen Alex pamoja na Frank kas na mwengine ambae hakufahamika jina Ni raia wa Nchini Kenya.

Ameongeza kusema kuwa majeruhi wengine 40 wanaendelea na matibabu hospitalini na hadi sasa Watu 6 wameruhusiwa kurudi majumban mwao huku 34 wakisalia hospitalin kwa matibabu zaidi.

Kamanda Khadija ametoa wito kwa Madereva kuheshimu sheria za barabaran ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika na kuwataka madereva wa vyombo vya moto kuheshimu upindo wa njia pamoja na kupunguza mwendo kasi wa gari zao pindi pale wanapokuwa barabarani.

Rauhiya Mussa Shaaban.