Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia kwa Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed imethibitisha kisa cha tatu cha Mgonjwa wa Corona na kufanya idadi ya walioambukizwa kufikia 14 kwa Tanzania.

Mgonjwa huyo ni mwanamke raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 57. Mwanamke huyo alirejea Zanzibar akitokea Uingereza na shirika la ndege la Qatar.