Taarifa rasmi: Serikali yapiga marufuku Bodaboda Zanzibar

Kutokana na kuongezeka kwa ajali za barabarani zinazotokana na uendeshaji wa Pikipiki maarufu Bodaboda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia bodi ya usafiri barabarani imepiga marufuku usafiri huo maarufu bodaboda kutumika kama chombo cha biashara visiwani Zanzibar.

Marufuku hiyo ya bodaboda imeanza leo Septemba 21, 2018 kama ilivyoelezwa na katibu wa bodi ya usafiri barabarani Mohammed Simba Hassani.

Kwamujibu wa kifungu namba 48 mabano 2 cha sheria ya usafiri barabarani, sheria namba 6 ya mwaka 2003 ni marufuku kwa mtu yeyote kutumia bodaboda au usafiri wa bodaboda kama ni chombo cha biashara.

kuanzia muda wa tangazo hili Serikali itaanza kufanya operasheni kwa maeneo yote ambayo kutakuwa na mkusanyiko wa vyombo vya moto vya bodaboda ambavyo vinadhamira ya kuwapakia wananchi kutoka sehemu moja na kuwapeleka sehemu nyengine.

Ndugu wananchi, ifahamike kwamba biashara ya bodaboda haijaruhusiwa kisheria na Serikali ya mapinduzi Zanzibar, kwahiyo mtu yeyote atakaye bainika anafanyabiashara  hiyo au mtu yeyote akibainika amekaa pahala  kwadhamira ya kufanya biashara hiyo. mtu huyo atakuwa amefanya kosa kwa mujibu wa ibara ya 48 mabano 2 na hatua kali za kisheria zitaanza kuchukuliwa.

Aidha katibu wa bodi ya usafiri barabarani Mohammed Simba amewataka wananchi kuacha kuutumia usafiri huo kwani Serikali bado inalitafakari kwa kina suala la usafiri wa bodaboda kutumika Zanzibar.