Leo Julai 22-2019 Majira ya Saa 4:00 Asubuhi Injinia Msaidizi wa Umeme katika Meli ya Mv. Mapinduzi II Haji Abdallah Khatibu mwenye umri wa miaka 55 amegundulika kuwa ameshajinyonga na kupoteza maisha ndani ya meli hiyo ambapo chanzo cha tukio hilo bado hakijatambulika.

Tukio hilo limetokea wakati Meli hiyo ikifanya safari zake za kawaida na ikitarajiwa kufika Pemba majira ya saa saba adhuhuri.

Kwamujibu wa taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu  Wizara ya Ujenzi  Mawasiliano na Usafirishaji  Zanzibar Mustapha Abdu Jumbe zinasema kuwa tukio hilo nimejiri  wakati meli hiyo ikiwa katika eneo la tumbatu kuelekea kisiwani Pemba na ilibidi safari isitishwe na meli ilirudi bandarini Unguja kwa Uchunguzi zaidi.

Amesema Serikali imeamua kusitisha safari hio kutokana na marehemu huyo ni mkaazi wa Kisiwa cha Unguja lakini pia Idara na vitengo muhimu wa uchunguzi vipo Unguja na ndio maana ikaharakishwa meli hiyo kurudi kwa haraka Zaidi kwa ajili ya uchanguzi.

Aidha alisema kuwa mara baada ya uwasili kwa mwili huo katika bandari ya malindi Unguja Maafisa kutoka jeshi la Polisi Unguja na vitengo vya upelelezi walifanikiwa kuingia katika chumba kilichotokea tukio hilo na kuchukua vieleezo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mwili wa marehemu huyo umepelekwa hospitai ya rufaa ya mnazi mmoja kwa ajili ya taratibu nyingine kuendelea.