Watu wasiopungua 10 wamefariki na wengine 50 kujeruhiwa baada treni ya abiria waliyokuwa wakisafiria kugongana na treni ya mizigo katika mji wa Rahim Yar Khan mashariki mwa Pakistan hivi leo asubuhi.

Kulingana n ripoti, treni hiyo ya abiria ilikuwa ikielekea kusini magharibi mwa mji wa Quetta kutoka mashariki mwa Lahore wakati ilipogongana na treni ya mizigo katika kituo cha reli cha Walhar huko Rahim Yar Khan katika mkoa wa Punjab.

Madaktari wamesema kuwa kuna uwezekano wa idadi ya vifo kuongezeka kwa sababu wengi wa waliojeruhiwa wako katika hali mahututi.