Mapema leo Septemba 14, 2018 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  imetangaza zawadi kwa mwananchi yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya usajili klabu ya Simba, Zacharia Hans Pope na Frankline Lauwo baada ya TAKUKURU kuwatafuta kwa njia za kawaida na kutowapata.

Image result for hans pope MAHAKAMANI

Mnamo April 30, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilitoa amri ya kukamatwa kwa Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo  na wafikishwe mahakamani ili kuunganishwa katika kesi inayomkabili Rais wa Klabu hiyo, Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

Amri hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao.

Wakili Swai alidai amewatafuta washtakiwa hao tangu Machi mwaka huu bila mafanikio hivyo akaomba hati ya kuwakamata washtakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani.

Chanzo: ITV Tanzania