Dawati la jinsia wanawake na watoto mkoa wa kusini unguja limesema idadi ya kesi za makosa ya udhalilishaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa mwaka 2018 imepungua  ukilinganisha na mwaka 2016 na 2017 katika mkoa huo.

Akizungumza wakati akitoa elimu juu ya adhari ya vitendo hivyo  kwa wanafunzi wa msingi  hadi secondari katika skuli ya kiongoni makunduchi na jambiani  mkuu wa dawati la jinsia mkoa wa kusini unguja  ndugu Ali Mohd Othman amesema mwaka 2016 jumla ya kesi zilizoripotiwa ni 132 mwaka 2017 kesi 168 na 2018 kesi 125  jambo ambalo limeonekana kupiga hatua  kubwa ya kupungua kwa vitendo vya uzalilishaji.

Amesema hatua hiyo imekuja kufuatia utekelezaji mzuri w mikakati waliojipangia katika dawati hilo kwa kushrukiana na watendaji wa mkoa  kwa kuwafikia wanafunzi wa skuli mbalimbali na madrasa kuelimisha mambo mbali mbali ikiwemo mbinu za kujiepusha na mazingira hatarishi yanayochangia kufanyika kwa vitendo hivyo.

Aidha amesema jeshi la polisi kwa sasa limejipanga vyema katka kushuhulikia makosa hayo ili kuona kwamba watenddewa wa vitendo hivyo wanapata haki hivyo amewahimiza wazazi na walezi kunga mkono jitihada hizo ili kuona kwamba vitendo hivyo vinaondoka kabisa

Ndugu ali amewataka wanafunzi kuongeza bidii katika masomo yao na kujiepusha na vishawishi mbali mbali vitavyopelekea kuharibu masomo ya kwa lengo la kufaulu vyema masomo yao na kujijengea mstakbali mzuri wa maisha yao ya baadae.

Nao wanafunzi hao kwa upande wao wamewaomba viongozi na watendaji wa serekali kuendelea kulishuhulikia  suala hilo pamoja  na kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa wale watakaobainika wametendand vitendo hivyo.