Katibu wa Mufti Zanzibar Khalid Mfaume Ali amesema  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bado haijarusu kufungua Madrasa za vyuo vya Qur-ani pamoja na Madrasa za watu Wazima.

Hayo ameyasema huko Ofisini kwake  Mazizini Mjini Zanzibar wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu tamko la kusimamisha Darsa za watu wazima pamoja na masomo ya madrasa (Qur-ani)

Amesema kufuatia tamko la kuruhusiwa shuhuli za kijamii kama vile harusi,na mambo mengine watu wengi walifahamu kuwa kila jambo lililokatazwa kutokana na maradhi ya Corona tayari limesharuhusiwa.

Aidha amesema Serikali imesema zilizoruhusiwa ni Skuli na sio madrasa  hivyo ziendelee kusubiri mpaka pale  maelekezo Mengine yatapotolewa.

Vile vile alisema kufunguliwa kwa Skuli haina maana kuwa ndio muhimu zaid kuluiko madrasa ila unatafutwa utaratibu maalum ili kuweka hali ya usalama .

Hata hivyo amewaomba masheha na walimu wote wa Madrasa waendelee kusubiri na kutoa mashirikiano na anaamini Wananchi wote watafuata kikamilifu maelekezo yaliyotolewa .