Mama mtoto wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna amelazimika kuzima skendo ya kudanganya tarehe ya kujifungua mtoto wao.

Kabla ya Tanasha kujitokeza na kuweka mambo sawa, mara tu baada ya kujifungua Oktoba 2, mwaka huu, zilisambaa taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa alidanganya kwani alishajifungua siku nyingi.

Diamond au Mondi ndiye aliyetangaza kuwa amebahatika kupata mtoto wa kiume na mpenzi wake, Tanasha katika tarehe hiyo ambayo na yeye amezaliwa.

Baadhi ya mashabiki walimjia juu na kutaka aache kudanganya watu kwani inaonesha mtoto alizaliwa siku kadhaa zilizopita.

Katika kuweka mambo sawa, Tanasha alitumia Insta Stories yake kuweka kibandiko maalum cha Hospitali ya Aga Khan jijini Dar alichovishwa mkononi kikionesha mtoto wake amezaliwa Oktoba 2, mwaka huu na namba ya kuzaliwa ni 158-03-1.

“Nimekaa leba kwa saa 17 na ujauzito wangu umedumu kwa wiki 42, nimejifungua kwa njia ya kawaida, sasa ni mama wa mtoto mzuri wa kiume anayeshea ‘birthday’ na mpenzi wangu (Diamond),” aliandika Tanasha.