TAASISI YA VIWANGO YA ZANZIBAR (ZBS)

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Viwango ya Zanzibar Na.1 ya 2011.

Lengo kuu la kuanzishwa Taasisi ya Viwango ya Zanzibar ni kuhakikisha kuwa Zanzibar inakua na viwango kwa ajili ya bidhaa na huduma na kusimamia ubora wa bidhaa na huduma hizo. Viwango na bidhaa zenye ubora zinalenga kulinda afya na usalama wa watumiaji pamoja na kukuza uchumi wa Zanzibar na kuhifadhi mazingira ya nchi.

Taasisi ya Viwango ya Zanzibar (ZBS) inakaribisha maombi ya kujaza nafasi tupu katika Idara zake kwa waombaji wenye sifa stahili katika Ofisi yake iliyopo Unguja.

Nafasi zenyewe ni kama zifuatazo:-

UNGUJA

 1. MKURUGENZI KATIKA IDARA YA HUDUMA ZA TAASISI
  Sifa za muombaji:
  i. Awe ni Mzanzibari.
  ii. Awe na elimu isiyopungua shahada ya pili katika fani ya uongozi, biashara, uchumi au sheria.
  iii. Awe na uwezo wa kufanya kazi bila ya kusimamiwa.
  iv. Awe na uwezo wa kusimamia na kuongoza.
  v. Awe na uzoefu wa kazi katika fani husika usiopungua miaka mitano.
  vi. Mwenye taaluma ya ziada kwenye fani husika atapewa kipaumbele.
  vii. Mshahara ni kwa mujibu wa ngazi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  viii. Awe tayari kufanya kazi muda wa ziada/ dharura.
 2. MKURUGENZI KATIKA IDARA YA MAENDELEO YA VIWANGO
  Sifa za muombaji:
  i. Awe ni Mzanzibari.
  ii. Awe na elimu isiyopungua shahada ya kwanza katika fani ya sayansi au uhandisi.
  iii. Awe na uwezo wa kufanya kazi bila ya kusimamiwa.
  iv. Awe na uwezo wa kusimamia na kuongoza.
  v. Awe na uzoefu wa kazi katika fani husika usiopungua miaka mitano.
  vi. Mwenye taaluma ya ziada kwenye fani husika atapewa kipaumbele.
  vii. Mshahara ni kwa mujibu wa ngazi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  viii. Awe tayari kufanya kazi muda wa ziada/ dharura.
 3. MKURUGENZI KATIKA IDARA YA USIMAMIZI WA UBORA
  Sifa za muombaji:
  i. Awe ni Mzanzibari.
  ii. Awe na elimu isiyopungua shahada ya kwanza katika fani ya sayansi au uhandisi.
  iii. Awe na uwezo wa kufanya kazi bila ya kusimamiwa.
  iv. Awe na uwezo wa kusimamia na kuongoza.
  v. Awe na uzoefu wa kazi katika fani husika usiopungua miaka mitano.
  vi. Mwenye taaluma ya ziada kwenye fani husika atapewa kipaumbele.
  vii. Mshahara ni kwa mujibu wa ngazi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  viii. Awe tayari kufanya kazi muda wa ziada/ dharura.

NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI
Muombaji anatakiwa aandike barua ya maombi na kuambatanisha vitu vifuatavyo:
a) Maelezo binafsi ya muombaji (CV). b) Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo. c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa. d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari. e) Picha moja ya Muombaji (Passport size) iliyopigwa karibuni. f) Majina na anuani za Wadhamini wawili wanaotambulika. g) Anuani rasmi anayopatikana muombaji, barua pepe na nambari ya simu.

MAMBO YA KUZINGATIWA
i. Muombaji atakaewasilisha “Statement of Result” au “Progressive Report” maombi yake hayatazingatiwa. ii. Muombaji anatakiwa aainishe nafasi moja anayoiomba kati ya zilizotajwa hapo juu vinginevyo maombi yake hayatazingatiwa. iii. Kwa Muajiriwa wa Serikali maombi yake yapitie kwa muajiri wake vinginevyo maombi yake hayatazingatiwa. iv. Barua za maombi ziandikwe kwa mkono na ziwasilishwe moja kwa moja Ofisi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar iliyopo Eneo la Viwanda Amani wakati wa saa za kazi. v. Siku ya mwisho ya kupokea maombi ni Ijumaa tarehe 21 Febuari, 2020 saa 9.30 alaasiri. vi. Mawasiliano yatafanywa kwa wale tu watakaopita katika mchujo wa awali (short listed).
Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:-
MKURUGENZI MKUU, TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR, S.L.P 1136, ZANZIBAR.

Tangazo hili linapatikana pia katika Tovuti ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) ambayo ni www.zbs.go.tz.