Tume ya Utumishi Serikalini inawatangazia wasailiwa wote watakaofanya usaili katika Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa upande wa Pemba wanatakiwa kufika kwenye usaili tarehe 17/11/2018 hadi tarehe 21/11/2018 kwamba, usaili huo hautafanyika katika Skuli ya Fidel Castro na badala yake utafanyika katika Ukumbi wa Benjamini William Mkapa Wete Pemba wakati wa saa 2:00 asubuhi.

Aidha, Tume ya Utumishi Serikalini inaomba radhi kwa usumbufu huo.

Ahsanteni