MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR (ZSSF) UNAWATANGAZIA WASTAAFU WANAOPOKELEA PENCHENI YA ZSSF KUPITIA BENKI TOFAUTI KUWA UHAKIKI KWA WANACHAMA SASA UTAFANYIKA MWANZONI MWA MWEZI WA JANUARI 2019

KWA WASTAAFU WOTE WA UNGUJA NA PEMBA UHAKIKI HUO UTAFANYIKA KUANZIA TAREHE 02 HADI 11 JANUARI 2019 KUANZIA SAA 2:00 ZA ASUBUHI 

UHAKIKI HUO UTAFANYIKA KATIKA AFISI ZA ZSSF KILIMANI MNARA WA MBAO NA TIBIRINZI CHAKECHAKE PEMBA.

AIDHA KWA WASTAAFU WALIOPO DAR ES SALAAM UHAKIKI WAO UTAFANYIKA KUANZIA 02/01/2019 HADI 05/01/2019 KATIKA AFISI ZA MRATIBU WA SHUGHULI ZA SMZ ZILIZOPO MTAA WA LITHULI MKABALA NA JENGO LA WIZARA YA FEDHA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

INASISITIZWA KUWA WASTAAFU WATAKAPOKWENDA KUHAKIKIWA WANATAKIWA KUCHUKUA VITAMBULISHO VYAO VYA ZSSF NA ASIYEHAKIKIWA PENCHENI YAKE ITAZUIWA.

AIDHA ZSSF INAWATANGAZIA WANACHAMA WAKE KUWA KWA SIKU HIZO ZA UHAKIKI (YAANI TAREHE 02 HADI 11 JANUARI 2019) HUDUMA ZA USAJILI WA WANACHAMA PAMOJA NA MAFAO ZITASITISHWA HADI KUMALIZIKA KWA ZOEZI LA UHAKIKI.

KILA ATAKAESIKIA TANGAZO HILI AMUARIFU MWENZIWE.