MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR (ZSSF)

S.L.P 2716

KILIMANI MNARA WA MBAO

 

MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR (ZSSF) UNAWATANGAZIA WASTAAFU WANAOPOKELEA PENCHENI YA ZSSF KUPITIA BENKI TOFAUTI KUWA UHAKIKI KWA WANACHAMA UMEWADIA.

KWA WASTAAFU WOTE WA UNGUJA NA PEMBA UHAKIKI HUO UTAFANYIKA TAREHE 02 JANUARI 2018 HADI 07/01/2018 KUANZIA SAA 2:00 ZA ASUBUHI.

UHAKIKI HUO UTAFANYIKA KATIKA AFISI ZA ZSSF KILIMANI MNARA WA MBAO NA TIBIRINZI CHAKECHAKE PEMBA.

INASISITIZWA KUWA UHAKIKI HUO NI KWA SIKU SITA TU. WASTAAFU WATAKAPOKWENDA KUHAKIKIWA WANATAKIWA KUCHUKUA VITAMBULISHO VYAO VYA ZSSF NA ASIYEHAKIKIWA PENCHENI YAKE ITAZUIWA.

AIDHA WASTAAFU WOTE AMBAO HADI LEO HAWAJAFUNGUA AKAUNTI ZA BENKI NA KUWASILISHA NAMBARI ZAO KWA AJILI YA KUPITISHIA MALIPO YAO YA PENCHENI ZSSF, WANATAKIWA KUHARAKISHA KUFANYA HIVYO. MNAARIFIWA KUWA HAKUTAFANYIKA MALIPO YEYOTE KWA NJIA YA FEDHA TASLIM KUANZIA MWEZI HUU WA JANUARI.

KILA ATAKAESIKIA TANGAZO HILI AMUARIFU MWENZIWE.

 

BODI YA WADHAMINI NA WAFANYAKAZI WA ZSSF WANAWATAKIA KHERI YA MWAKA MPYA WA 2018 NA UWE WENYE MAFANIKIO

 

LIMETOLEWA NA:

 MKURUGENZI MWENDESHAJI

MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR,

S.LP 2716

 

SIMU: +255 – 24 – 2230242

FAKSI: +255 – 24 – 2232820

Zanzibar

Barua pepe: info@zssf.org

Kilimani Mnara wa Mbao,

Plot. No: 51

Zanzibar – TANZANIA

 

ZSSF NI UFUNGUO WA MAISHA YA BAADAE