Serikali haitasita kuchukua hatua kwa mwananchi yeyote ambaye atakamatwa akichimba mchanga maeneo yasiyoruhusiwa.

Hiyo ni kauli iyo tolewa na Mkuu wa Wilaya ya Wete, Abeid Juma Ali baada ya kukamata zaidi ya tani 15 za mchanga ulikua katika maandalizi ya kusafirishwa kutoka bonde la Gawani Shehia ya Jadida wilaya ya wete.

Alisema uchimbaji mchanga umewekewa utaratibu maalumu ili kuhakikisha rasilimali hiyo inaendelea kutumika kwa manufaa ya umma.

“Hatuwezi kufumbia macho vitendo hivi, tutahakikisha mhusika akipatikana anachukuliwa hatua za kisheria,”alisema.

Ofisa Mdhamini Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Pemba, Sihaba Haji Vuai, alisema mchanga huo utataifishwa na kuahidi kuendelea kuwatafuta waliohusika na uchimbaji wa mchanga katika eneo hilo.

Alisema licha ya wahusika kutofahamika, lakini wizara itautaifisha mchanga huo wakati wanaendela kuwatafuta waliohusika na uharibifu huo.

Chanzo: ZanzibarLeo