Serikali ya Tanzania imesaini mkopo wa Sh3.3 trilioni kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) awamu ya pili kutoka Morogoro, Makutupora na Singida.

Akitoa maelezo kuhusu mkopo huo Waziriwa Fedha wa Tanzania Dkt Phili Mpango alieleza kwamba Serikali itazitumia fedha hizo kukamilisha mradi wa SGR katika maeneo yaliyopangwa.

Mkopo huo umetolewa kwa kuratibiwa na benki ya Standard Chartered na umehusisha wakopeshaji kumi na saba ikiwemo nchi ya Denmark.