Tanzania yapigwa na chini michuano ya mpira wa meza Rwanda, wachezaji wadai kukosa maandalizi ndio sababu

Wachezaji watanzania wametoa maoni yao baada ya kufanya vibaya kwenye mashindano ya mpira wa meza uliohusisha wachezaji walio chini ya umri wa miaka 18 ambapo bingwa katika mashindano hayo ni wenyeji Rwanda kwa wanaume na Eritrea kwa wanawake.

Baada ya kutofanya vizuri kwa timu ya Taifa ya Tanzania ya Mpira wa Meza chini ya miaka 18 kwenye mashindano ya vijana ya Afrika mashariki na kati yaliofanyika Kigali nchini Rwanda, Haya hapa ni maoni ya wachezaji wenyewe wamezungumzia sababu za msingi zilizopelekea Tanzania kuwa wasindikizaji kwenye mashindano hayo.

Mchezaji Mwanajuma Bakar na Sultan Suleiman wamesema mashindano hayo ni magumu sana huku wakisema walikosa maandalizi imara ndio maana hawakufanikiwa kupata kikombe hata kimoja.

Kwa upande wake mkuu wa msafara wa wachezaji hao pia ni mjumbe wa chama cha mpira wa Meza Zanzibar (ZTTA) Abubakar Khatib Kisandu, amesema ni faraja kubwa kwa kuona vyama vyao viwili vya ZTAA na TTA vinakuwa na mashirikiano ili kupata wachezaji wenye sura ya Tanzania ambapo Zanzibar na Tanzania bara wote wametoa wachezaji wao walioshiriki kwa pamoja katika michuano hiyo.