Tanzania imekabidhiwa tuzo maalum ya pongezi kutoka Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) baada ya kufanikiwa kuwa miongoni mwa mataifa 24 yanayoshiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON zitakazoanza kutimua vumbi Ijumaa wiki hii.

Tanzania imekabidhiwa cheti hicho wakati wa semina elekezi iliyoandaliwa na CAF kwaajili ya kuwakumbusha taratibu mbalimbali za kimashindano.

Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta ndiye aliyepokea tuzo hiyo kwa niaba ya msafara mzima wa Tanzania kwenye mashindano hayo.

Pia hapo jana kambi ya Taifa Stars imepokea ugeni mzito wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ambapo pamoja na mambo mengine amezungumza machache na wachezaji.