Tanzania imetoa muda wa nyongeza kwa wageni kukaa nchinin hiyo nia baada ya Kuwepo na mlipuko wa Ugonjwa wa Corona nakusababisha baadhi ya Wasafiri kushindwa kusafiri kurudi kwao .

Wageni ambao Pasi zao sa Kusafiria zimeisha muda au zinakaribia kuisha muda na hawawezi kusafiri kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID19 wanatakiwa kwenda Kituo chochote cha karibu cha Uhamiaji ili kuongezewa mwezi 1 wa bure kwenye Pasi zao za kusafiria

Hata hivyo kama hali hii itaendelea baada ya kuisha kwa mwezi 1 wa nyongeza, Wageni hao watatakiwa kufika katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji yaliyopo Kurasini, Dar es Salaam

Kwa wale wenye Kibali cha Ukazi, Pasi ya Kusafiria ya Wageni, ‘Exemption Certificate’ na Dependant Pass ambazo zimeisha muda wamepewa mwezi 1 wa nyongeza kukaa nchini. Lakini muda huo ukikaribia kuisha wanashauriwa kufika Makao Makuu ya Uhamiaji