Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imesema tatizo la wizi wa simu nchini umepungua  baada ya kuzima namba tambulishi bandia.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar meneja wa mawasiliano nchini TCRA Inocent Mongi amesema tatizo hilo limepungua baada ya wananchi kutoa taarifa polisi na kapmuni ya simu husika kwa kuzimwa kwa namba tambulishi ya simu iliyopotea.

simu feki

Zaidi ya simu million moja laki saba zimezimwa na TCRA kuanzia tarehe 16-29 mwezi june mwaka huu ili kuongeza usalama mtandaoni kwa watumiaji wa simu ,kudhibiti wizi wa simu na kuzuwia matumizi ya simu zisizokuwa na kiwango.

 

NA:FAT HIYA SHEHE ZANZIBAR24